Tous les cantiques

Unakuja, ee mwokozi, unakuja, mfalme

Kolwezi

Paroles

Couplet 1

Unakuja, ee Mwokozi, unakuja, Mfalme,

Kila ulimi takiri Jina Lako, ee Bwana;

Unakuja, tutaimba kwa furaha na shangwe.

Safari yetu ‘takwisha, tutakaa na Wewe.

Refrain

Unakuja, unakuja tutakuona Bwana,

Unakuja, unakuja Tutafanana Nawe;

Unakuja, unakuja Yesu Bwana Mpendwa:

Furaha gani kuona uso Wako, ee Bwana.

Couplet 2

Unakuja siku ile utafuta machozi,

Zambi, shida na mateso hayo yote ‘takwisha;

Tutaiacha dunia na mambo yake yote,

Tutayasahau yote itakuwa furaha.

Refrain

Unakuja, unakuja tutakuona Bwana,

Unakuja, unakuja Tutafanana Nawe;

Unakuja, unakuja Yesu Bwana Mpendwa:

Furaha gani kuona uso Wako, ee Bwana

Couplet 3

Unakuja mawinguni pamoja na malaika,

Kwa sauti Yako kubwa wafu watafufuka,

Na sisi tulio hai, o tutabadilika,

Sote tutanyakuliwa kukutana na Wewe.

Refrain

Unakuja, unakuja tutakuona Bwana,

Unakuja, unakuja Tutafanana Nawe;

Unakuja, unakuja Yesu Bwana Mpendwa:

Furaha gani kuona uso Wako, ee Bwana

Couplet 4

Unakuja, twakungoja, tunajua ni kweli,

Hatujui siku na saa, twajua u karibu;

Unakuja, tutakula mezani Nawe Bwana

Kwa Karamu ya Arusi Yake Mwana Kondoo.

Refrain

Unakuja, unakuja tutakuona Bwana,

Unakuja, unakuja Tutafanana Nawe;

Unakuja, unakuja Yesu Bwana Mpendwa:

Furaha gani kuona uso Wako, ee Bwana