Siku moja nitamwona Bwana
Nyimbo za Wokovu · n° 99
Paroles
Wokovu 99 - Siku moja nitwamwona Bwana
Couplet 1
Siku moja nitamwona Bwana Yesu uso wake. Na milele kwa furaha nitaka’ karibu naye.
Nitamtazama Yesu ju’ ya nyota zote pia, huko kwa ukamilifu nitajua nguvu yake.
Couplet 2
Hapa ninaufahamu kwa sehemu wema wake, huko nitamtazama na kushiba kwa kuona.
Nitamtazama Yesu ju’ ya nyota zote pia, huko kwa ukamilifu nitajua nguvu yake.
Couplet 3
Shangwe gani kwa Yesu! Shida zote zitaisha, giza haitakuwapo, na huzuni itakoma.
Nitamtazama Yesu ju’ ya nyota zote pia, huko kwa ukamilifu nitajua nguvu yake.
Couplet 4
Yesu atafika mbio, Lo! Mwenyewe atashuka! Tutanyakuliwa juu ili kumlaki Bwana.