Tous les cantiques

Tukienda pamoja kushikana na Mungu

Nyimbo za Wokovu · n° 166

Paroles

Wokovu 166 - Tukienda pamoja, kushikana

Couplet 1

Tukienda pamoja, tukishikamana na Mungu, tunapata amani na raha; tukifanya daima yanayompendeza, yu karibu kutusaidia.

Raha, furaha twazipata kwa Yesu, tukidumu katika kuamini, kutii.

Couplet 2

Ikiwapo dhoruba, na mawimbi ya’vuma, yanakoma kwa neno la Yesu. Tukiona jaribu na kuhofu adui, tutashinda kwa nguvu ya Yesu.

Raha, furaha twazipata kwa Yesu, tukidumu katika kuamini, kutii.

Couplet 3

Tukibeba mizigo anatustarehesha, tunapata furaha halisi. Masumbuko yatoka, giza inageuka kuwa nuru njiani mwa Mungu.

Raha, furaha twazipata kwa Yesu, tukidumu katika kuamini, kutii.

Couplet 4

Tuna raha ya Mungu katika mashindano tukitii na tukiamini. Jua lake la pendo linawaangazia watiio na waaminio.

Raha, furaha twazipata kwa Yesu, tukidumu katika kuamini, kutii.