Ninakumbuka sayuni nchi ya heri mbinguni
Nyimbo za Wokovu · n° 84
Paroles
Wokovu 84 - Ninakumbuka Sayuni
Couplet 1
Ninakumbuka Sayuni, nchi ya heri Mbinguni, bahari kama kioo na’furahia rohoni. Nyuma kimeta cha nuru Naona mji wa Mbingu, nyimbo za nyumba ya Baba nasikiliza daima.
Mapambazuko Mbinguni yataondoa utaji, vyote tulivyoamini tutaviona milele.
Couplet 2
Mauti haina nguvu, Yesu a’vunja uchungu, naye aliwakomboa wote; wafalme, watumwa. Ninamtwika Mwokozi dhambi, huzuni na shida; mbavuni mwake nafasi kama bandari salama.
Mapambazuko Mbinguni yataondoa utaji, vyote tulivyoamini tutaviona milele.
Couplet 3
Kuna ’jaribu njiani, mengi yakunizuia, na mara nyingi miiba, inaumiza miguu. Nikikumbuka Sayuni moyo huwaka kabisa, Mbingu ninaitazama na ku’himiza safari.
Mapambazuko Mbinguni yataondoa utaji, vyote tulivyoamini tutaviona milele.