Hakuna aliye fika
Iz'i Gisenyi · n° 99
Paroles
Hakuna aliye fika pale Kaluvari, akarudi tena ginsi alivyo kuwa mbele.
Couplet 1
Paulo alipokutana naye Yesu, alirudi amekwisha badilika, akafikiya kusema si mimi niishiye, kwani Bwana pekee akiishi ndani yangu.
Hakuna aliye fika pale Kaluvari, akarudi tena ginsi alivyo kuwa mbele.
Couplet 2
Pale kisimani, mwanamke Msamariya alipokutana na Muumbaji wake, alipewa Maji iletayo Uzima, akarudi amekwisha badilika.
Hakuna aliye fika pale Kaluvari, akarudi tena ginsi alivyo kuwa mbele.
Couplet 3
Ukiwa musherati, usikate tama, uje kwake Bwana Atakupokea, maana Alisema njooni kwangu nyinyi wote munaolemewa na mizigo yenu.
Hakuna aliye fika pale Kaluvari, akarudi tena ginsi alivyo kuwa mbele.
Kwa maana: Yeye Ndiye kimbilio mwamba wetu Wakaribu.
Hakika ndugu: Yeye Ndiye Musahada usio kosekana.
Kwa magonjwa: katika vidonda Vyake tunapata Uponaji.
Ukiwa na kiu: Yeye Ndiye chemuchemu ya Maji ya Uzima.
Leta hitaji Répéter 2 fois
yako ndugu, leta hitaji yako kwa Yesu, naye Atakupa jibu.
Leta mzigo Répéter 2 fois
wako ndugu, leta mzigo wako kwa Yesu, naye Atakupumuzikisha.
Leta shida Répéter 2 fois
yako ndugu, leta shida yako kwa Yesu, naye Atakupa jibu.
Leta magonjwa Répéter 2 fois
yako ndugu, leta magonjwa yako kwa Yesu, utapata Uponyaji.