Tous les cantiques

Ukiona kiwu sana ujalivu wa mwokozi

Nyimbo za Wokovu · n° 282

Paroles

Wokovu 282 - Ukiona kiu sana ujalivu wa Mwokozi

Couplet 1

Ukiona kiu sana ujalivu wa Mwokozi, roho yake safi pia, liamini neno la babako na atakujazi, nawe utashangilia.

Atakujaliza hata utashiba. Bwana Yesu akuita: "Njoo bila ’sitasita!" Atakujaliza hata utashiba Roho na uwezo wake.

Couplet 2

Vichukue vyombo vyako, uvioshe safi sana kisimani pa Golgotha! Afadhali kujitoa lote kwa Mungu Bwana, na imani itaota.

Atakujaliza hata utashiba. Bwana Yesu akuita: "Njoo bila ’sitasita!" Atakujaliza hata utashiba Roho na uwezo wake.

Couplet 3

Na mafuta ya Neema hayakomi. Asifiwe! Tunakuwa na shukrani! Anataka kumimina Roho ya ahadi yake. Mpokee kwa imani!

Atakujaliza hata utashiba. Bwana Yesu akuita: "Njoo bila ’sitasita!" Atakujaliza hata utashiba Roho na uwezo wake.